Friday, October 1, 2010

ZIJUE SALA WAKATI WA KUVAA MAVAZI YA IBADA

SALA ZA MWANAIBADA ANAPOVALIA KWA IBADA
(Sala zinazoendana na Mavazi ya Ibada ya Padre anapokuwa anajiandaa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu.)

Amictus:
Ee Bwana univishe kofia ya chuma ya wokovu ili nipigane dhidi ya mashambulio ya mwovu.
Place this helmet of salvation upon my head so as to enable me to overcome the assaults of the devil.

Alba:
Ee Bwana unioshe mimi na usafishe roho yangu, Nipate kuoshwa katika damu ya mwanakondoo, Na hivyo nipate kufurahia furaha ya milele.
Cleanse me Lord and purify my heart so that being made white in the blood of the lamb, I may have the fluition of everlasting joy.

Cingulum:
Ee Bwana nifunge mimi na mshipi wa usafi na uzime viunoni mwangu tamaa mbaya na hivyo niwe ndani yangu na tunu za kujitawala na usafi wa moyo.
Guard me Lord with this guard of purity and extinguish from my loins every desire of lust that the virtues of countenance and chastity may ever abide in me.

Stola:
 Ee Bwana unijalie Stola ya umilele ambayo ilipotezwa kwa dhambi ya wazazi wetu wa kwanza, japo sistahili kulijongea fumbo lako takatifu, unistahilishe kupokea raha ya milele.
Restore to me this Stole of immortality upon me, which I lost by the fall of our first parents, and although I am unworthy as I approach this Sacred Mystery I may be found worthy of everlasting joy.

Casula:
 Ee Bwana uliyesema “Nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi” nijalie nguvu ya kuuchukua, niweze kupata neema zako.
Lord you said that your yolk is easy and your burden is light; enable me to bear it as to obtain thy favour.








From St Andrew’s Missal

No comments:

Post a Comment